Obama anahimiza uchimbaji mafuta

Rais Obama ametangaza hatua mpya za kuzidisha sekta ya mafuta nchini humo.

Katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio, alisema uchimbaji wa mafuta huko Alaska na Ghuba ya Mexico, hatimaye utasaidia kuacha kutegemea sana mafuta kutoka nchi za nje.

Siku za nyuma Bwana Obama akipendelea kutafuta njia mpya za kutoa nishati, bila ya kuchafua mazingira.

Lakini hivi sasa Wamarekani wanalalamika juu ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Wapinzani wa Rais Obama, wa chama cha Republican, wamekuwa wakidai kuwa sekta ya uchimbaji mafuta nchini Marekani kwenyewe itanuliwe.