Wapalestina wanaandamana

Askari wa usalama wa Israil na waaandamanaji wa Palestina wamepambana ufukwe wa magharibi wa mto Jordan, wakati Wapalestina wanakumbuka kuundwa kwa taifa la Israil, mwaka wa 1948, ambapo Wapalestina wengi wakawa wakimbizi.

Haki miliki ya picha Getty

Katika eneo la Gaza, inaarifiwa watu kama 15 walijeruhiwa na mizinga na bunduki za rashasha.

Katika ufukwe wa magharibi, kwenye mji wa Ramallah, mamia ya polisi wa Israil wa kupambana na fujo pamoja na jeshi, walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za mpira dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.

Piya kuna taarifa kuwa risasi zilifyatuliwa katika milima ya Golan, wakati wakimbizi wa Kipalestina walioko Syria, walipovuka mpaka.

Piya watu zaidi ya 10 wamejeruhiwa kutokana na risasi, katika tukio kama hilo kwenye mpaka wa Israil na Libnan.