Rais mpya wa Ivory Coast ameapishwa

Miezi sita baada ya uchaguzi uliokuwa na mzozo, rais mpya wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, ameapishwa.

Haki miliki ya picha AP

Sherehe zilizofanywa mji mkuu, Yamoussoukro, zilihudhuriwa na viongozi wengi wa Afrika pamoja na Rais Sarkozy wa Ufaransa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.

Bwana Uottara aliushukuru ulimwengu kwa kumuunga mkono , na alisema kwamba kauli ya wananchi wa Ivory Coast imeshinda.

Piya alitoa wito kwa watu kuonesha udugu na mapatano, na aliahidi kuwa ataongoza kwa niaba ya taifa zima.

Mwandishi wa BBC mjini Abidjan anasema, kazi kubwa inayomkabili Bwana Outtara ni usalama na uchumi.