Mapigano ya Abyei Sudan yanaendelea

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa mapigano kusitishwa katika jimbo lenye mafuta la Sudan, Abyei, ambako mapigano yamendelea kwa siku ya tatu.

Duru za Sudan Kusini zimeiambia BBC kwamba vijiji kaskazini ya mji wa Abyei, vilishambuliwa kwa mizinga na ndege.

Mapambano yalianza Alkhamisi, dhidi ya msafara wa Umoja wa Mataifa uliokuwa unawasindikiza wanajeshi wa eneo la kaskazini, ambapo wanajeshi wawili waliuwawa.

Jimbo la Abyei linaaniwa baina ya kabila la Dinka la Sudan Kusini na wachungaji wa Misseriya kutoka Sudan Kaskazini.

Pande zote mbili zinasaidiwa na majeshi ambayo yalipigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 20.