Utaratibu wa kukabili hatari ya nuklia

Viongozi wa Japan, Uchina na Korea Kusini, wamekubaliana kuanzisha utaratibu wa kuzinduana mapema, pakitokea hatari kwenye mitambo yao ya nuklia.

Image caption Mtambo wa nuklia Japan

Makubaliano hayo yamefikiwa miezi miwili baada ya kinu cha nishati cha nuklia cha Fukushima, Japan, kuharibika katika tetemeko la ardhi, na tsunami iliyofwata.

Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan, alikubali hatua hiyo baada ya mkutano mjini Tokyo, na Waziri Mkuu wa Uchina, Wen Jiabao, Rais Lee Myung-bak, wa Korea Kusini.

Viongozi hao watatu, walisema ulimwengu unafaa kujifunza kutoka janga hilo la nuklia la Japan.