Birmingham yafuta safari ya Tanzania

City Haki miliki ya picha Reuters (audio)
Image caption Birmingham City

Birmingham City wameamua kufuta safari yao ya kwenda Tanzania.

City, ambao wameshuka daraja katika ligi kuu ya England msimu huu walikuwa wasafiri kwenda Tanzania kupambana na Simba ya Yanga katika mechi za kirafiki.

Hata hivyo watayarishaji walishindwa kuthibitisha utaratibu wa safari hiyo katika muda waliopewa.

Mabingwa hao wa kombe la Carling sasa wanatafuta nchi ya kwenda kucheza mechi za za kalba ya kuanza kwa msimu.