Ukame unatishia kati na mashariki Uchina

Serikali ya Uchina inasema watu karibu milioni 35 sasa wameathirika na ukame mkubwa kabisa kutokea katika kipindi cha miaka 50, katika majimbo ya kati na mashariki.

Haki miliki ya picha AP

Wakuu wa bwawa la Mabonde Matatu, llinalozalisha umeme kwenye mto wa Yangtze, wanasema pengine hawatoweza kumwaga maji zaidi kwa wakulima, ikiwa mvua haitonyesha katika majuma mawili yajayo.

Kuna upungufu wa umeme na watu zaidi ya milioni 5 wanakosa maji ya kunywa ya kutosha.

Wavuvi wengi wametafuta kazi mijini kwa sababu kina cha maji kwenye maziwa kimepungua na samaki wanakufa.

Mazao yakikauka katika eneo hilo linalotoa nafaka nyingi, basi na bei ya vyakula itazidi kupanda.