Mubarak atozwa faini dola milioni 90

Mahakama ya Misri yameamrisha faini ya dola milioni 90, atozwe rais wa zamani, Hosni Mubarak, pamoja na maafisa wake wawili, kwa kukata huduma za simu za mkononi wakati wa maandamano dhidi ya serikali mwezi wa Januari.

Haki miliki ya picha AFP

Hiyo ndiyo hukumu ya mwanzo ya mahakama dhidi ya Bwana Mubarak.

Kiongozi huyo wa zamani anakabili mashtaka makubwa zaidi, kama kuamrisha waandamanaji kuuwawa, ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifo.

Maafisa wawili waliotozwa faina na Bwana Mubarak ni waziri mkuu wa zamani, Ahmed Nazif, na waziri wake wa mambo ya ndani ya nchi, Habib al-Adly.