Watazamaji mechi wameuwawa Burundi

Watu wane wamekufa nchini Burundi wakati watu waliokuwa na silaha, walipofyatua risasi dhidi ya mkahawa nje ya mji mkuu, Bujumbura, jana usiku.

Baadhi ya ripoti zinasema hao ni wafuasi wa kikundi kipya cha wapiganaji, na walilenga mkahawa huo kwa sababu uko karibu na ofisi ya chama tawala cha CNDD-FDD, na ulijaa watu waliokuwa wakitazama mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.