Vettel ashinda mashindano ya langalanga

Sebastian Vettel wa Timu ya magari ya Red Bull ametumia fursa ya mtafaruku uliotokea kwenye mbio za mashindano ya magari ya Langalanga huko Monaco mapema leo na kujishindia mbio hizo akifuatiwa na Fernando Alonzo wa magari ya Ferrari na Jenson Button wa McLaren akimaliza wa tatu.

Image caption Sebastian Vettel

Huu ni ushindi wa tano kwa Vettel kati ya mbio sita za Msimu huu akitetea ubingwa aloutoa mwaka jana.

Mpinzani wake wa karibu Lewis Hamilton wa Timu ya magari ya McLaren aliyemshinda kwenye mbio za Uchina hakuwa miongoni mwa gari ya mwanzo baada ya hapo jana kushindwa kufuzu vizuri katika mbio za mwisho za mchujo na vilevile kupokonywa pointi akilazimika kuanza katika nafasi ya tisa asubuhi ya leo.

Dereva huyo Mjerumani alitumia mbinu isiyokubalika kwa kusisitiza kutumia ma tairi mepesi kwa mzinguko 15 akishindana na Fernando Alonzo wa magari ya Ferrari aliyeonyesha nia yake ya kutumia ujanja kurejesha matumaini ya Timu yake kupiga hatua na kuhesabiwa katika mashindano ya magari ya Langalanga.

Button wa magari ya Mclaren aliyemaliza nyuma ya magari hayo mawili alisema baada ya mbio kwamba kuwafuata madereva hao na kuona jinsi walivyoshindana ilikuwa faraja kwake kusubiri ijitokeze fursa labda niwapiku.

Msisitizo wa kutumia tairi nyeesi ilikuwa na hatari yake kwa dereva Vettel lakini bahati yake ilijitokeza kufuatia ajali kwenye mzunguko wa 72 ambapo Vettel aliweza kubadili tairi za gari lake bila kupoteza mda na kujikuta katika nafasi yake ile ile ya uongozi. Vettel alisema baada ya kumaliza kileleni kuwa nilisumbuliwa na dereva wa Ferrari Fernando Alonzo kwa takriban mizunguko 20 lakini hilo halikuniondolea ushindi.

Kwa kumaliza katika nafasi ya pili, Alonso leo amejisafisha baada ya Msaimu mzima kudorora bila kuelekea kupata ushindi na kuiacha Timu nzima ya Ferrari ikijiuliza tatizo liko wapi.

Dereva pekee ambaye alitarajiwa kumpa Sebastien Vettel msukumo Lewis Hamilton alimaliza wa sita licha ya kuamrsihwa kufanya mzunguko kwa kosa la kuligonga gari la Felipe Massa wa Timu ya magari ya Ferrari.

Hamilton alikuwa katika nafasi ya tisa ikisalia mizunguko saba kufikia mwisho wa mbio za leo kabla ya Algwesari wa magari ya Toro Rosso kulikwaruza gari lake ilibidi lifanyiwe ukarabati kabla ya Hamilton kuendelea na safari amalize wa sita.

Kwa ushindi huu Sevbastien Vettel amekusanya jumla ya point 143

Hamilton anafuata kwa pointi 85, Mark Webber wa Red Buill 79, Jennson Button 76.

Mashindano yatakayofuata yatakuwa ya Canada ambapo mbio za kuchuja gari la kuanza mbio yafanywe tareh 10 juni na mbio zenyewe jumapili tareh 12 juni.