Ocampo: Kenya inazinga uchunguzi

Mkuu wa mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, ameishutumu serikali ya Kenya, kuwa inafanya kampeni, ya kuzuwia uchunguzi juu ya ghasia zilizofuatia uchaguzi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Luis Moreno Ocampo

Mkuu huyo wa mashtaka, Luis Moreno-Ocampo, alisema, serikali inaleta hali ya khofu.

ICC imewashtaki wana-siasa na wafanya-biashara sita, kwa kuchochea ghasia hizo, zilizofuata uchaguzi wa mwaka wa 2007, ambapo watu zaidi ya elfu-moja walikufa. Wote wanakanusha mashtaka hayo.

Serikali ya Kenya imekuwa ikipinga hatua ya ICC, kwa sababu inasema mahakama ya Kenya yenyewe, yanaweza kusikiliza kesi hizo.