Watu wa Malta wakubali talaka

Watu wa Malta wamekubali kuwa talaka ikubalike katika sheria za nchi hiyo.

Image caption Wanandoa

Huo ndio ulikuwa uamuzi wa watu walioshiriki katika kura ya maoni iliyofanywa jana.

Akitangaza matokeo hayo, Waziri Mkuu, Lawrence Gonzi, alisema matokeo hayo siyo aliyotaraji, lakini aliahidi kuwa mswada utaoruhusu mke na mume kuachana, utapelekwa mbele ya bunge.

Malta na Philippines na Vatikani ndio nchi zilizobaki duniani, zinazopiga marufuku talaka.