Wapiganaji wateka Zinjibar, Yemen

Taarifa za kutatanisha kutoka Yemen zinasema watu mia kadha wenye silaha, wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Al Qaeda, waliuteka mji wa Zinjibar kusini mwa nchi baada ya mapigano makali ya siku mbili.

Haki miliki ya picha REUTERSAmmar Awad
Image caption Maandamano Yemen

Lakini upinzani wamemshutumu Rais Saleh, kuwa alikabidhi mji huo kwa makundi yake yenye silaha, kuzua picha kuwa Al Qaeda imehusika.

Bwana Saleh amedai kwa muda mrefu kuwa yeye pekee ndiye anaweza kupambana na Al Qaeda nchini Yemen.

Mchambuzi mmoja mjini Sanaa aliiambia BBC, kwamba makundi hayo yenye silaha siyo ya Al Qaeda, na kwamba wanajeshi wa serikali waliondoka Zinjibar bila ya kupigana.