Huwezi kusikiliza tena

Upinzani na vyombo vya sheria Tanzania

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ambaye alikamatwa na polisi mjini Dar es Salaam kwa madai ya kuruka dhamana hatimaye alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi iliyopo Arusha kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumatatu.

Bw Mbowe alitiwa mbaroni na polisi ambao wanadai walikuwa wakitekeleza amri ya mahakama iliyotoa hati ya kumkamata. Hata hivyo kumekuwa na malumbano nchini humo kuhusu utaratibu wanaotumia polisi kuwakamata wabunge wa upinzani.

Hadi sasa wabunge wanane wa upinzani wameshakamatwa kwa makosa mbalimbali.

Kutoka Dar es Salaam mwandishi wetu John Solombi aliandaa taarifa.