Kijiji chengine chashambuliwa Syria

Taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa wanajeshi wameingia katika kijiji chengine ili kuzima upinzani dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Haki miliki ya picha AP

Wanaharakati wanaopinga serikali wanasema vifaru na wanajeshi waliofyatua bunduki za rashasha waliingia Bdama, karibu na mpaka wa Uturuki.

Taarifa moja inasema watu kama mia moja walikamatwa.

Na Uingereza imewashauri wananchi wake waliobaki Syria, afadhali waondoke.