Jivu la Chile linafika Australia

Jivu la volcano iliyoripuka Chile limevuka bahari ya Pacific, na kuchafua safari za ndege nchini New Zealand na mashariki mwa Australia.

Maelfu ya abiria wamenasa na hata safari nyingi za ndani na nje ya nchi hizo zimesimamishwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa safari za ndege za Australia kuathirika na jivu la volcano katika kipindi cha miaka 20, na inafikiriwa hali hiyo inaweza kuendelea kwa siku kadha.

Upepo mkali umepeperusha jivu hilo kwa zaidi ya kilomita elfu tisa kutoka Amerika Kusini hadi Australia.