Kusafisha Fukushima kumeshindikana

Wahandisi katika kinu cha umeme cha nuklia cha Fukushima nchini Japan, wamesimamisha kazi ya kusafisha miyale katika maji katika kinu hicho, masaa tu baada ya kuanza, kwa sababu ya miale kuzidi.

Haki miliki ya picha Reuters

Mtambo huo una kinu chenye tani laki moja ya maji, ya kutosha kujaza mabwawa 40 ya kuogelea, ambacho kilijengwa wakati wa juhudi za kuupoza mtambo ulipoharibika kwenye tetemeko la ardhi na tsunami mwezi wa Machi.

Kampuni ya umeme iliyohusika, TEPCO, ilisema ikiwa kazi hiyo haitoanza tena juma lijalo, inaweza kuwa shida kuyasafisha maji hayo ambayo yanaweza kuvuja baharini.