Erdogan anamsihi Gaddafi aondoke

Madaktari katika mji wa Libya wa Misrata, ambao una bandari, wanasema mji huo umeshambuliwa tena na wanajeshi wa Kanali Gaddafi. Inaarifiwa kuwa watu kama 30 wameuwawa.

Haki miliki ya picha AFP

Na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameimbia televishjeni ya Uturuki, kwamba amependekeza kwa Kanali Gaddafi kwamba akiamua kuondoka Libya, anamuahidi kuwa atamsaidia kumpeleka kokote atakako.

Bwana Erdogan anasema hakupata jawabu:

"Sasa Muammar Gaddafi hatokezi hadharani, lakini watu wanaomzunguka, na watoto wake wanashughulika na mambo haya.

Wanapinga haya mabadiliko.

Lakini hana la kufanya ila kuondoka Libya, ikiwa atapewa ahadi.

Tumempa ahadi, yaani tumemwambia kwamba tuko tayari kumsaidia kusafiri kwenda kokote kule anakotaka.

Ikitegemea jawabu yake kwa wito wetu, tungejadili swala hili na washirika wetu, lakini kwa bahati mbaya, hatujasikia kitu kutoka kwake hadi sasa."