Mfalme anapendekeza mabadiliko Morocco

Viongozi wa wanaharakati wanaotaka mabadiliko nchini Morocco wanapanga kufanya maandamano Jumapili, ingawa Mfalme Mohammed ametangaza mabadiliko ya katiba.

Mfalme wa Morocco alisema mabadiliko anayopendekeza yatapunguza madaraka yake na kuzidisha nguvu za waziri mkuu na bunge.

Wadadisi wanataka katiba mpya iandikwe na kamati itayochaguliwa siyo wajumbe wataoteuliwa na mfalme.

Watu wengine wameyakaribisha mapendekezo hayo, na maelfu ya wananchi walitoka mababarani baada ya hotuba ya mfalme Ijumaa usiku, wakipepea bendera na kupiga honi za magari.