SADC inataka katiba mpya Zimbabwe

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, SADC, wanakutana mjini Johannesburg, kutafuta mwongozo utaoisaidia Zimbabwe kufikia uchaguzi ulio salama na wa kidemokrasi.

Jumuiya ya SADC inashikilia kuwa Zimbabwe iwe na katiba mpya kabla ya uchaguzi, lakini Rais Robert Mugabe anasema anataka uchaguzi ufanywe haraka iwezekanavyo.

Na Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai, ambaye miaka miwli iliyopita alijumuika na Bwana Mugabe kuunda serikali, anasema uchaguzi haufai kufanywa kabla ya kuwa na katiba mpya.