Rais wa Yemen hajulikani aliko

Waziri Mdogo wa habari wa Yemen amekanusha ripoti kuwa Rais Saleh ameondoka nchini, baada ya kujeruhiwa jana katika shambulio la kombora dhidi ya ikulu, katika mapigano baina ya jeshi la rais na watu wa makabila yanayompinga.

Haki miliki ya picha AFP

Baada ya kujeruhiwa jana, Rais Saleh alizungumza kusema kuwa ni mzima, lakini kuna tetesi nyingi nchini Yemen, kuhusu hali yake.

Shirika la habari la taifa limearifu kuwa maafisa kadha ambao walijeruhiwa pamoja na Rais Saleh, wamepelekwa Saudi Arabia kwa matibabu.

Marekani imelaani ghasia hizo na imetaka pande zote mbili zikabidhiane madaraka kwa amani.