Aliyedai kubakwa Libya aenda Marekani

Eman Haki miliki ya picha Other
Image caption Eman al Obeidi

Mwanamke mmoja nchini Libya ambaye alisema amebakwa na wafuasi wa Kanali Muammar Gaddafi ameondoka magharibi mwa Libya kuelekea nchini Marekani Kwa mujibu wa dada yake.

Eman al-Obeidi alikuwa akitoka katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi hadi mjini Washington DC, alisema dada yake Marwa.

Yaliyomsibu

Kisa cha Eman al-Obaidi kilifahamika pale alipokimbilia katika hoteli ya Rixos mjini Tripoli mwezi March na kuwaelezea waandishi wa habari wa kigeni waliokuwa katika hoteli hiyo hiyo yaliyomsibu. Mapema wiki hii , bi Obeidi alirejeshwa Tripoli kutoka Qatar.

Haki miliki ya picha l
Image caption Eman al Obeidi

Aliomba ukimbizi huko, baada ya ya kutioka Libya, kupitia Tunisia.

Dada yake bi Obeidi, Marwa alisema shirika la kutetea haki za binadamu likisaidiwa na waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton lilikuwa limewaandalia Ema na baba yake ndege binafsi ambayo ingewapeleka mjini Washington, kupitia Malta na Austria.

Pia alisema maafisa wa Qatar walikuwa wema kwa dada yake hadi saa chache kabla ya kumrejesha Libya. "Tunataka tu fursa kwake ya kupatiwa matibabu ya kisaikolojia na apumzika" alilieleza shirika la habari la Associated Press. " dada yangu amepitia mengi " alisema maafisa wa Qatar walikuwa wema kwa dada yake hadi saa chache kabla ya kumrejesha Libya.

Kutoroka

Wakati bi Obeidi akielezea taarifa yake kwa waandishi wa habari mwezi March, wafuasi wa serikali walimvuta na kumsukuma mbali. Alipotea kwa siku kadhaa kabla ya kuonekana nchini Tunisia.

Bi Obeidi alisema alisaidiwa na askari walioasi kutoroka.