Tanzania yaelekea kufuzu kwa Olimpiki

Tanzania imeimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki baada ya kuilaza Nigeria 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Haki miliki ya picha aboodmsuni.blogspot.com
Image caption Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wasiozidi umri wa miaka 23

Thomas Ulimwengu aliifungia Tanzania bao hilo la ushindi dakika 8 kabla ya mechi kumalizika.

Nigeria ambayo ilionekana kudhibiti mchezo huo kwa asilimia kubwa ilipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Watashinda

Kocha wa Nigeria Austin Eguavoen, amesema licha ya kushindwa kwao katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza, ana matumaini

makubwa kuwa vijana wake watashinda mechi ya marudiano itakayochezwa mjini Abuja baadaye mwezi huu.

Lakini kocha wa Tanzania, Jamhuri Kihwelu, ana wingi wa matumaini kuwa kikosi chake kina uwezo wa kuwashinda miamba hao

wa Nigeria, katika mechi ya raundi ya pili, baada ya vijana hao wa Taifa Stars kuwaondoa washindi wa medali ya

Haki miliki ya picha aboodmsuni.blogspot.com
Image caption Kocha wa Tanzania

dhahabu katika mashindano hayo ya olimpiki, Cameroon.

Afrika Kusini ambayo imeandikisha matokeo mema mwaka huu, ni miongoni mwa timu ambazo zilipoteza mechi zao za

ugenini.

Afrika Kusini ililazwa 3-1 na Benin.

Matokeo mengine

Kwa wakati mmoja Afrika Kusini ilikuwa ikiongoza 1-0 bao lililofungwa na nyota wao Bongani 'Drogba' Ndulula.

Lakini Benin ilifunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa mchezaji Fadel Suanon, dakika 3 tu kabla ya kipindi cha

kwanza kumalizika.

William Dassagate naye akaongeza bao la tatu kunako kipindi cha pili.

Ilikuwa ni wikendi mbovu kwa mataifa ya Kusini mwa bara Africa, Zambia nayo ililazwa 3-0 na Algeria.

Ivory Coast ilitoka nyuma ya 1-0 na kuishinda Congo 2-1 mjini Brazzaville. Kufuatia ushindi huo Ivory Coast

inakaribia kufuzu kwa raundi ya mwisho ya mashindano hayo itakayochezwa mwezi Desemba mwaka huu.