2.6 milioni ni wapiga kura hewa Zimbabwe

Image caption Masanduku ya kupigia kura Zimbabwe

Orodha ya wapiga kura iliyofichuliwa katika daftari la kudumu la wapiga kura nchini Zimbabwe imebaini kuwa majina ya wapiga kura hewa milioni 2.6 yamejumuishwa kwa dhamira ya kuendeleza udanganyifu, haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika moja linaloheshimiwa sana nchini Afrika Kusini.

Orodha hito inaashiria kuwa kuna zaidi ya watu alfu 41 walio na umri wa zaidi ya miaka mia moja-hii ikiwa ni mara nne zaidi ya idadi ya watu hao nchini Uingereza, ambayo ina idadi kubwa zaidi ya watu na muda mrefu wa kuishi ikilinganishwa na Zimbabwe.

Rais Robert Mugabe ameitisha uchaguzi ufanyike mwaka huu.

Lakini mpinzani wake wa siku nyingi, na waziri mkuu katika serikali ya mseto, Morgan Tsvangirai, amesema kuwa uchaguzi huo unapaswa kuandaliwa mwaka 2012 baada ya katiba mpya kuidhinishwa ili kuhakikisha kuwa kuna uhuru na haki.

Uchaguzi wa mwaka 2008 ulikumbwa na vurugu dhidi ya wafuasi wa bwana Tsvangirai, na wachambuzi wamedai kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa katika kura za hapo awali.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka kati ya wafuasi wa Bw Mugabe na Bw Changirai katika siku za hivi karibuni huku uchaguzi huo ukikaribia.

Siku moja ya kuzaliwa

Bw Johnson amesema serikali ya zimbabwe imekuwa ikijaribu juu chini kuweka siri orodha hiyo ya wapiga kura lakini alifanikiwa kupata nakali ambaye ameifanyia uchumbuzi kwa nia ya shirika la linalohusiana na uhusiano baina ya watu wa rangi mbali mbali, South African Institute of Race Relations.

Image caption Bw Mugabe na Bw Tsvangirai

Ametaja kwamba ingawa Zimbabwe umri wa kuishi miongoni mwa raia wa Zimbabwe imeteremka hadi miaka 49, kulikuwa na wapiga kura 41,100 wanaodaiwa kuwa na zaidi ya umri wa miaka 100.

Kadhalika aligundua kuwa watu 16,800 walikuwa na siku moja ya kuzaliwa - Tarehe 1 Januari mwaka 1901, huku majina ya watu walioaga dunia hayajaondolewa kwenye orodha hiyo.

Wapiga 230 walikuwa na umri wa chini ya miaka 18, na baadhi yao walikuwa na chini ya umri wa miaka miwili.