Homa ya E Coli yapungua

Waziri wa afya wa Ujerumani anasema kuwa visa vipya vya homa hatari ya E coli vinapungua kwa kiwango kikubwa hivyo kwa wakati huu hali yaitishi sana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wauguzi wamhudumia mgonjwa wa E coli

Waziri Daniel Bahr ana amini kuwa homa hiyo imefika upeo wake lakini anaonya kuwa vifo zaidi vinatarajiwa kutokana na visa vipya vinavyochipuka.

kufikia sasa watu 24 wamefariki kutokana na homa hiyo ya E coli huku wengine 2,400 wakiambukizwa na mamia wakiachwa na matatizo ya figo.

Awali Umoja wa Mataifa ya Ulaya ulipendekeza wakulima walipwe jumla ya Euro milioni 150 kama fidia.

Lakini mawaziri wa kilimo wa mataifa hayo walipinga wakisema wanataka kima hicho kiongozwe ili wakulima wa matunda na mbonga waweze kufidiwe kikamilifu kutokana na hasara waliopauta ambayo inakisiwa kufikia Euro milioni 417m kwa wiki.

Wiki iliyopita maafisa wa afya kutoka ujerumani walidai kuwa mkurupuko wa homa hiyo ya E coli eti ulikuwa kumesababishwa na matango ya kihispania.Lakini sasa imebainika kuwa matango hayo sio chanzo cha homa hiyo.