Afrika Mashariki yakabiliwa na Njaa

Shirika moja la kimarekani limeonya kuwa janga kuu la uhaba wa chakula duniani linaendelea kubana mashariki mwa upembe wa Afrika.

Image caption Uhaba wa chakula waathiri Afrika Mashariki

Shirika hilo lijulikanalo kama The Famine Early Warning Systems Network limeonya kuwa nchi zinazotia wasiwasi ni Ethiopia, Kenya na Somalia.

Limesema usaidizi mkubwa wa dharura unahitajika kuokoa maisha na kukabiliana na utapiamlo katika eneo hilo.

Shirika hilo pia limesisitiza kuwa usaidizi unaotolewa kwa sasa hautoshi.

Katika taarifa yake shirika hilo limesema kuwa eneo la upembe wa afrika limeathiriwa na upungufu wa mvua kwa misimu miwili hivyo kusababisha ukame mbaya zaidi tangu mwaka 1995