Malawi yazuwia ruzuku za wagonjwa wa HIV

Serikali ya Malawi imesimamisha kutoa ruzuku maalum kwa watumishi wa serikali wenye virusi vya HIV na UKIMWI kwa sababu inasema wanatumia fedha hizo kwa kunywa pombe na kuwapa makahaba.

Image caption mchango kwa wagonjwa wafujwa

Takriban watumishi wa serikali elfu 40 wamenufaika na mpango huo.

Serikali ya Malawi inawashtumu watumishi wa serikali nchini humo kwa kueneza zaidi virusi vya HIV na UKIMWI Kwa kutumia fedha hizo kujihusisha na vitendo vinavyohatarisha maisha.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Makahaba hupokea fedha za msaada

Kuanzia sasa kila mwezi watapokea posho ya chakula cha lishe bora badala ya kupokea fedha za ziada.

Afisa moja asema mpango huo umetumiliwa vibaya zaidi na watumishi wa serikali wanaojidai kua nao pia wamambukizwa na virusi vya HIV ili wajipatie fedha zaidi..Takriban asilimia 15 ya wakaazi wa Malawi wana virusi vya HIV,na idadi kubwa ya vifo kutokana na ugonjwa huo umepunguza kiwango cha maisha kufikia umri wa wastani wa miaka 36 tu