Rais wa Somalia aeleza kifo cha Fazul

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ametoa maelezo zaidi kuhusu kuuawa kwa kiongozi wa Al Qaeda Afrika Mashariki, Fazul Abdullah Mohammed, ambaye alipigwa risasi mjini Mogadishu siku ya jumatano.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa Somalia

Rais wa Somalia alisema Marekani ilisaidia kuthibitisha utambulisho wa mtu huyo, na ukaguzi ulifanywa nje ya nchi.

Aliwaonesha waandishi wa habari, ile ambayo alisema, ni hati ya kuzaliwa ya Fazul Abdullah Mohammed, picha za familia yake, na ramani ya pengine malengo ya kushambulia mjini Mogadishu.

Haki miliki ya picha other
Image caption Aliahidi kushambulia Mogadishu

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, ambaye yuko Tanzania - akitarajiwa leo kuweka shada la mauwa kwenye jengo la ubalozi wa Marekani, lililoshambuliwa kwa bomu na Al Qaeda mnamo mwaka wa 1998, kwenye operesheni, ambayo Marekani inasema, ilipangwa na Fazul Abdullah Mohammed.