Makabiliano yaendelea mjini Zawiya Libya

waasi Libya Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Makabiliano makali yanaendelea mjini Zawiya

Makabiliano makali kati ya waasi na wanajeshi wanaomtii kanali Muammar Gaddafi yanaendlea mjini Zawiya.

Mji huo wenye utajiri wa mafuta ulioko magharibi mwa mji kuu Tripoli, ulitekwa na waasi mwezi Machi lakini wanajeshi wa serikali walifaulu kuutwa tena baada ya makabiliano makali.

Jeshi la Gaddafi hata hivyo limesema linafanikiwa kuwakabili waasi mjini humo.

Waasi wanasemekana kupata nguvu kufuatia mashambulizi yanayoendelea kutoka ndege za kijeshi za NATO ambazo zimefanya uharibifu mkubwa kwenye ngome za jeshi la kanali Gaddafi.

Huku makabiliano yakienedelea, runinga ya kitaifa imeonyesha picha ya Kanali Gaddafi akiwa anacheza mchezo of chess na kiongozi wa chama cha kimataifa cha mchezo huo. Waandishi wanasema hii ni ishara kuwa Gaddafi hana nia ya kutoka mamlakani.

Wakati huo huo mapambano makali pia yanaendelea mjini Misrata ambapo madaktari wanasema watu sita wameuawa na wengine kumi na sita wamejerihiwa vibaya.

Wanajeshi wamewazingira waasi kwenye pembe tatu za mji huo lakini bandari bado ipo wazi na inatumika kuwahami waasi.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema mashambulio ya NATO yamewapa nguvu waasi kusonga mbele zaidi.

Kufikia sasa NATO wametekeleza jumla ya mashambulizi elfu nne dhidi ya jeshi la Gaddafi.

Mapambano yaliozuka mjini Zawiya yanaonyesha kuwa makamanda wa jeshi la serikali wamechanganyikiwa na hawajui waweke vikosi vyao maeneo yapi ilikufaulu dhidi ya waasi.