Waliobakwa Libya hatarini

Kanali Gaddafi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanali Gaddafi

Wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Libya wanaonya kuwa wanawake ambao wamekuwa wajawazito baada ya kubakwa wakati wa mzozo wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na watu wa familia zao.

Onyo hilo linakuja baada ya mashirika kadhaa ya misaada magharibi mwa Libya kusema kuwa mauji hayo ndiyo sababu kuu ya watu kukimbilia nchini Tunisia.

Ubakaji mwiko

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imesema inaamini vikosi vya kanali Gaddafi na waasi wanatumia ubakaji kama silaha ya vita.

Waandishi wa habari wanasema, ingawa suala la ubakaji ni jambo la aibu kuzungumziwa kote duniani, nchini Libya suala Libya suala hilo ni mwiko kutajwa hadharani.