Vikosi haviondoki Libya

Mkuu wa majeshi ya Uingereza amesema kuwa operesheni za vikosi vyake huko Libya hauna kikomo na utaendelea kulingana na mahitaji.

Hayo ni baada ya wasiwasi kuzushwa na mkuu wa jeshi la maji.

Image caption Mkuu wa jeshi la Uingereza

General Sir David Richards ameiambia BBC kuwa tuna uwezo wa kuendeleza operesheni hii kwa mda wowote na tutakavyoona.

Nato ilichukuwa jukumu la kusimamia mapigano nchini Libya kuanzia tarehe 31 March, mwanzoni ikiwa ni kwa kipindi cha siku 90 lakini sasa mda huo umezidishwa kwa siku 90 zaidi.

Image caption Jeshi la maji la Uingereza

Mkuu wa Jeshi la maji, Navy chief Admiral Sir Mark Stanhope alisema kuwa mtazamo wa operesheni lazima ubadilike endapo mpango mzima ukizidi miezi sita.

Mpango wa Nato kuweka eneo marufuku juu ya safari za ndege kupaa kwenye anga ya Libya kulisababishwa na kiongozi wa Libya mwenyewe, Kanali Mummar Gaddafi aliyejibu maandamano kwa mkono wa chuma wakipinga utawala wake wa miaka 41.