Afrika Kusini tayari kuandaa CAN -2013

Rais wa shirikisho la soka nchini Afrika Kusini, (Safa) amesema taifa hilo liko tayari kuchukua mahala pa Libya na kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la taifa bingwa barani afrika mwaka wa 2013.

Image caption Uwanja wa Port Elizabeth nchini afrika Kusini

Shirikisho la mchezo wa soka branai Afrika CAF limekiri kuwa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya, umeilazimisha shirikisho hilo kuchunguza upya jinsi ya kuandaa mashindano hayo ikiwa mzozo huo utaendelea kwa muda mrefu.

Nematandani amesema Safa litaiandikia CAF baadaye wiki hii kuwasilisha nia yake.

Mapema mwaka huu, Afrika Kusini, iliandaa fainali za kuwania fainali zakombe la taifa bingwa barani Afrika kwa wavulana wasiozidi umri wa miaka 20 baada ya maandamano ya kisiasa kuanza nchini Libya.

Image caption Shabiki wa soka wa timu ya taifa ya Afrika Kusini wakati wa fainali za kombe la Dunia mwaka wa 2010

Vyombo kadhaa vya habari vinasema, wenyeji hao wa kombe la dunia mwaka wa 2010, tayari wamepewa nafasi hiyo ya kuwa mwenyeji wa fainali hizo kombe la taifa bingwa barani Afrika za mwaka 2013, lakini Nematandani amesema habari hizo sio za kweli.

Baadaa ya kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka uliopita, AfrikaKusini, tayari imepangiwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka wa 2017.

Uamuzi huo sasa huenda ukanyeuka ikiwa CAF itaamua kuwa fainali za mwaka wa 2013 zitaandiliwa nchini humo, lakini Nematandani amesema wao wako tayari kwa mashauriano zaidi.

Afrika Kusini iliwania nafasi ya kuandaa fainali hizo za mwaka wa 2015 lakini CAF ikaamua nafasi hiyo kutwaliwa na Morocco.