Assad awataka waliokimbia warudi

Rais Hafidh al Assad amewasilisha hotuba yake ya kwanza baada ya kipindi cha miezi miwili ya ukimya katikati ya vuguvugu la mwamko wa wananchi wake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Assad

Rais huyo kijana alirithi madaraka kutoka kwa babake amehimiza utashi wa mabadiliko ya kisiasa katika hotuba aliyoitoa mbele ya wafuasi wake katika Chuo Kikuu cha Damascus, ingawa hakukuwa na dalili kama atajiuzulu.

Katika mji mkuu Damascaus, wananchi waliipokea kwa hisia mbalimbali.

Katika hotuba yake amesema kuwa mdahalo wa Kitaifa ndiyo utakaounda njia na hali ya baadaye ya Syria na wakati huo huo kuwataka raia wa Syria waliokimbilia Uturuki warejee nyumbani.

Punde baada ya hotuba yake ikaarifiwa maandamano katika miji kadhaa ya nchi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption waandamanaji mjini Damascus

Walioshuhudia wanasema kuwa mojapo ya maandamano yalifanyika katika kiunga cha mji mkuu Damascus, ambako watu waliishutumu hotuba wakisema hatutaki mdahalo na wauwaji, kwa mujibu wa shirika la habari Reuters.

Mashirika ya haki za binadamu yanasema takriban raia 1,300 wameuawa kufikia leo kutokana na maandamano ya kuipinda serikali mnamo mwezi march na askari wapatao 300 na polisi kuuawa.

Kwa mda sasa waandamanaji wameisha onyesha kuwa hawataki mjadala na kwamba wana amini wakuu wa nchi hawataki mabadiliko ya aina yoyote kutoka nchini na wafaa kungolewa madarakani na wawajibikishwe.

Hotuba ya Bw.Assad inatokea wakati Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kuandaa pendekezo la azimio la kutaka vikwazo zaidi dhidi ya Syria.

Huku nyuma watu waliokimbia vurumai ya majeshi kaskazini magharibi mwa Syria wanasema kuwa Syria imekata mawasiliano kutoka mji wa Bdama ambako misaada ilikuwa ikipitia kuwafika wakimbizi hao na familia zao.

Akizungumza kwenye televisheni mbele ya wafuasi wake katika chuo kikuu cha Damascuss, Bw.Assad alionyesha masikitiko yake juu ya vifo akisema kuwa ni hasara kubwa kwa taifa na kwake binafsi.

Hata hivyo alisema wachocheza wa ghasia waliolichafua jina la Syria kote kupitia maandamano watatengwa.

Amewataka wananchi wake wakubali mdahalo kujadili masuala mengi ikiwa ni pamoja na rushwa na kuongezea kuwa kamati kuhusu mjadala wa Kitaifa imeundwa na vilevile kuwa ameiomba wizara ya sheria kuweka msamaha kwa raia wote. Halikadhalika amewataka maelfu ya wakimbizi walioko Uturuki waliokimbia kwa hofu ya maisha yao warejee majumbani mwao haraka iwezekanavyo.