Porto Andre Villas-Boas kuongoza Chelsea

Kocha wa Porto coach Andre Villas-Boas anatarajiwa kujiunga na timu ya Chelsea kufwatia kufutwa kazi kwa Carlo Ancelotti mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Wachezaji wa Porto na kocha wao Villa-Boas wakisherekea ushindi wao katika fainali ya kombe la UEFA.

Villas-Boas mwenye umri wa miaka 33 alisaidia Porto kushinda ligi ya Europa msimu uliopita.

Kuna sehemu kwenye mkataba wake na Porto inayomruhusu kuondoka iwapo kuna timu itakayotoa pauni za Uingereza milioni £13.2m kwa huduma yake.

Porto imekanusha madai hayo

Katika taarifa, Porto wamesema hawajapata ombi la kuweza kumruhusu kocha huyo.

" Kwa sasa timu hii haijapata mawasiliano yoyote ya kuweza kumruhusu kuondoka,au makubaliano na kocha huyo,"taarifa ilisema.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Kocha mteule wa Chelsea Villas-Boas

Chelsea inasema itatoa tangazo kuhusu meneja wake katika siku chache zijazo.

Rais wa timu ya Porto Pinto da Costa amesema hawatomzuia Villas-Boas kuondoka iwapo kiasi cha fedha wanachohitaji kitatolewa.

"Villas-Boas ana mkataba na sehemu ya mkataba inayozungumzia euro milioni 15m," alithibitisha. " Kama mtu ataweka euro milioni 15m kwenye akaunti yetu na anataka kuondoka,hatuwezi kufanya lolote kwa kuwa ni suala ambalo limewekwa wazi kwenye mkataba."