Nilidanganywa kukimbilia Saudi-Ben Ali

ben Ali Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa Rais wa Tunisia Ben Ali

Rais wa Tunisia aliyeondolewa madarakani Zine al-Abidine Ben Ali amesema hakuwa anakimbia nchi wakati alipoondoka mwezi Januari

Katika taarifa iliyotolewa wakati wa kesi yake ikianza kusikilizwa huku yeye mwenyewe akiwa hayupo Ben Ali alisema aliichukua familia yake na kuipeleka Saudi Arabia kwa ajili ya usalama.

Bwana Ben Ali alisema alikuwa na nia ya kurejea Tunisia haraka lakini ndege ilimuacha kwa ‘kutokutii maagizo yangu.’

Alisafiri kwenda Saudi Arabia Januari 14 kufuatia mapinduzi ya kiraia

"Nilidanganywa kuondoka Tunisi" alisema bwana Ben Ali.

Alikana pia mashtaka kuwa alitoa amri ya kuwafyatulia risasi waandamanaji, kitu ambacho anasema kingeweza kuthibitishwa kwa mawasilaino yaliyorekodiwa kati ya Rais, waziri wa mambo ya ndani

na wizara nyingine.

Lakini mwandishi wa BBC John Leyne anasema kwa wakti huu hayo sio mashataka yake ya msingi.

Kesi ya sasa inaangalia mashataka dhidi ya ufisadi na uuzaji wa dawa za kulevya, ambayo yote Rais huyo wa zamani ameyakanusha.

Iwapo atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kutokana na tuhuma mbali mbali ikiwemo rushwa na uuzaji wa dawa za kulevya.

Wanasheria wake wanasema kesi yake ilikuwa ni njama za serikali ya mpito ya Tunisia kupumbaza watu wasiihoji kwa kushindwa kurejesha utulivu na utengamano wa nchi

Mamlaka ya Saudia haijajibu chochote kuhusu ombi la Tunisia kuwa Bwana Ben Ali na mkewe Leila Trabelsi warejeshwe Tunisia na kuna dilili kidogo za wao kuletwa mbele ya mahakama kukutana na

mkono wa sheria.

Mamlaka ya Tunisia imekuwa ikitayarisha mashtaka kadha ya kisheria dhidi ya Ben Ali, lakini kusikilizwa kwa kesi yake Jumatatu hii kutaanza na tuhuma dhidi ya pesa, silaha na dawa za kulevya,

ambazo anatuhumiwa kuziacha katika kasri lake kabla hajakimbia.