Maofisa wa upinzani Libya ziarani Uchina

Mahmoud Jibril Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahmoud Jibril

Afisa wa ngazi ya juu anayeshughulikia mashauri ya kigeni katika upinzani wa Libya amewasili Uchina kwa mazungumzo na serikali ya nchi hiyo.

Mahmud Jibril anatazamiwa kujadili jinsi ya kukomesha mgogoro nchini Libya, ambako Uchina ina hamu ya mafuta ya petroli.

Uchina inafuata ilichokiita sera ya kutoingilia masuala ya wengine pamoja na kutopendelea upande wowote katika masuala yanayoendelea katika nchi nyingine.

Wakati wa kura kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuamua kuishambulia Libya, kwa kutumia vikosi vya NATO na tangu hapo imeshutumu mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na majeshi hayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uchina ilipinga hatua ya NATO

Halikadhalika Uchina haijashiriki miito ya kumtaka Kanali Gaddafi ajiuzulu.

Hata hivyo, ziara ya Bw.Jibril kwa mujibu wa mwandishi wetu mjini Beijing itaonekana kama pigo jingine kwa Bw.Gaddafi na utawala wake.

Katika siku za hivi karibuni Uchina imekuwa ikijitahidi kuzipatanisha pande mbili zinazozozana huko Libya.

Maofisa wa Uchina wameisha fanya mikutano miwili na Mkuu wa Baraza la mseto la Libya, Mustapha Abdul Jalil.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Libya, Abdelati al-Obeidi, pia alikuwa mjini Beijing kwa siku tatu mapema mwezi huu ambapo Uchina ilizungumzia kusitisha mapigano kama muhimu kwa pande zote mbili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption wa Libya wakiandamana Uchina

Uchina huenda ikatafakari kutoa mchango wa fedha kwa waasi. Italy,Ufaransa,Kuwait na Qatar zimejitolea kutoa mchango.

Uchina inaendesha biashara ya mafuta nchini Libya na iliwaondoa takriban wafanyakazi wake 30,000 mwanzoni mwa mwaka huu machafuko yalipozuka mnamo mwezi February.