Waasi wakaribia Tripoli

Wanajeshi wa waasi nchini Libya Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanajeshi wa waasi nchini Libya

Majeshi ya waasi magharibi mwa Libya yanasema kuwa yameendeleza mashambulio dhidi ya vikosi vinavyo muunga mkono Kanali Gadaffi katika mji muhimu kilomita 80 Kusini mwa mji mkuu wa Tripoli.

Msemaji wa jeshi hilo aliyeko katika eneo la milima ya Nafusa, amesema kuwa kumekuwa na makabiliano makali tangu siku ya Jumapili pembezoni mwa mji wa Bair al-Ghanam hadi maeneo ya Kusini Magharibi.

Hata hivyo msemaji wa Jeshi la serikali, Mousa Ibrahim, amesema kuwa mji wa Tripoli bado umeshikiliwa na kiongozi wa taifa hilo Kanali Muammar Gadaffi anayeendesha shughuli za serikali japo alikataa kuthibitisha iwapo bado Gadaffi yupo mjini Tripoli.