River Plate yashushwa daraja-Argentina

Ghasia zimeibuka katika mji mkuu wa Argentina, Buenos Airies, kufuatia kuondolewa kwa moja ya klabu kongwe zaidi nchini humo, River Plate kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 110 ya historia yake.

Haki miliki ya picha riverplate.com
Image caption Wachezaji wa Klabu ya River Plate

Madaktari wanasema zaidi ya watu 25 walijeruhiwa baada ya mashabiki wa River Plate kukabiliana vikali na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria nje ya uwanj wa nyumbani wa klabu hiyo ya River Plate.

Awali polisi walitumia vitoa machozi na magari ya kurusha maji kuwatawanya mashabiki hao ambao walivamia uwanja kama mechi kati ya River Plate na Belgrano de Cordoba inaendelea, hatua iliyosabisha mechi hiyo kusitishwa dakika ya mwisho.

Haki miliki ya picha Riverplate.com
Image caption Mchezaji wa River Plate akisherekea kufunga bao.

River plate ilihitajika kushinda kwa zaidi ya mabao mawili lakini timu hiyo ikatoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na klabu ya Belgarda de Cordoba.

Mechi hiyo iliendelea chini ya ulinzi mkali na duru zinasema zaidi ya maafisa wa polisi 2000 walishika doria.

Kuanzia msimu ujao klabu hiyo sasa itashiriki ligi daraja ya pili hatua iliyosababisha mashabiki wa klabu hiyo kuzua rapsa, kayika mji mkuu wa nchi hiyo.

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Argentina linachunguza tukio hilo, na klabu hiyo inakabiiwa na adhabu kali zaidi mbali na kuondolewa kwenye ligi kuu.