Kombe la Dunia la wanawake

Michuano ya Kombe la Dunia kwa kina dada imeanza leo nchini Ujerumani.

Image caption Kombe la Dunia kwa kina dada

Nigeria imecheza na Ufaransa, na kufungwa bao 1-0.

Bao la Ufaransa lilipatikana katika kipindi cha pili, kupitia Marie-Laure Delie katika dakika ya 56.

Mechi rasmi ya kuyafungua mashindano hayo ni kati ya wenyeji Ujerumani dhidi ya Canada mjini Berlin.

Vile vile ikiwa katika kundi A, Nigeria itakutana na wenyeji Ujerumani, ambao pia ni mabingwa watetezi, na baadaye kucheza dhidi ya Canada.

Hadi sasa zaidi ya tiketi 900 zimeisha nunuliwa kujionea michuano ya Kombe la Dunia la wanawake, hilo linatosha kuonyesha jinsi gani mashindano haya yalivyovutia wengi.

Wenyeji wa mashindano haya Ujeremani wamejitahidi kuleta sura ya tafrija ambayo iliwezesha mashindano ya mwaka 2006 ya Kombe la Dunia kwa wanaume kutia for a.

Mashindano haya yamepewa umihimu mkubwa na kutoa fursa za kuweka runinga kwenye vituo mbalimbali vya hadhara ili wapenzi wa soka wasikose uhondo popote walipo katika miji mbalimbali.

Hata hivyo hamu ya wenyeji wa mashindano haya ni Timu yao ya Taifa ambayo inatazamia ushindi wa Kombe la wanawake kwa mara ya tatu mfululizo.

Uwezekano wa kuandaa fainali hii ya Kombe la Dunia kwa wanawake ulipewa msukumo na mwanaume.

Mkuu wa Chama cha mpira cha Ujerumani Theo Zwanziger ambaye ametoa wito kwa Wajerumani waheshimu soka ya wanawake.

Jumla ya Timu 16 ndiyo zilizofuzu kwa fainali hizi zitakazofanyika kwenye viwanja vya miji tisa.

Pamoja na wenyeji Ujerumani, Marekani pamoja na Brazil ni Timu za kuangaliwa kwa uwezo wao wa kumaliza kwa ushindi.

Licha ya wababe hao kila Timu inayoshiriki inaweza kuharibu matarajio ya wengi.

Wakati huu ambapo idadi ya wanawake wanaocheza soka imeongezeka kote duniani, pamoja na uwekezaji kuzidishwa katika soka hio, kuna imani kubwa kuwa fainali ya mwaka huu ya Kombe la Dunia la wanawake itatoa sura ya kiwango cha maendeleo kilichofikiwa.

.