Mali na Mauritania wapambana na al Qaeda

Askari wa vikosi vya Mauritania wakishirikiana na wa Mali wamevamia kambi ya Al Qaeda iliyoko magharibi mwa nchi ya Mali, kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.

Image caption operesheni Al Qaeda

Duru za usalama kutoka Mali zimesema kuwa mapigano makali yalitokea kwenye kituo kilichoko katika msitu wa Wagadou mnamo siu ya ijumaa, ikiwa na silaha nzito zilitumiwa.

Wagadou, eneo lililo karibu na mpaka wa Mauritania ni eneo linalofahamika kuwa linatumiwa na tawi la mtandao wa al-Qaeda.

Mapema mwezi huu, nchi hizo mbili, Mali na Mauritania ziliafikiana kuongoza vikosi vya pamoja katika operesheni ya kukabiliana na chimbuko hili la al-Qaeda.

'majeruhi wamehamishwa' Shambulio lilifanyika jioni siku ya ijumaa na lilishirikisha mashambulizi ya anga, kwa mujibu wa duru zilizolifahamisha shirika la habari la Ufaransa,AFP zikiwa nchini Mauritania.

Duru hizo zimesema kuwa gaidi hao walijibu kwa silaha nzito".

Image caption Mtandao wa Al Qaeda

Hasara kamili kwa adui haijafahamika ingawa imetajwa kuwa kubwa. Hema zilizokuwa ndani ya kambi hiyo na magari matatu yaliteketezwa.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa wamedhibiti hali ya mambo katika eneo hilo.

Duru kutoka Mali zimesema kuwa walitumia helikopta kutoka Mali kuondoa majeruhi kutoka medani ya mapigano.

Serikali za mitaa zimekua katika hali ya tahadhari tangu kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden auawe nchini Pakistan mnamo mwezi May mwaka huu.

Kundi la Al-Qaeda katika eneo la Maghreb (AQIM) limefanya mashambulizi ya mara kadhaa pamoja na kuteka raia wa Ulaya waliokuwa katika eneo hilo.