Joto laathiri bahari

Bahari ya pembe ya kaskazini ya dunia
Image caption Bahari ya pembe ya kaskazini ya dunia

Wanasayansi wanaochunguza eneo la barafu la ncha ya kaskazini ya dunia, wanasema habari ya barafu imeyayuka kwa kadiri ambayo inaruhusu mimea na viumbe vya bahari hiyo kuingia katika bahari ya Atlantic, kwa mara ya kwanza katika miaka elfu kadha.

Wanasema mabadiliko hayo yataathiri mazingira ya bahari ya Atlantic.

Bahari ya pembe ya kaskazini ya dunia ilikuwa daima imefunikwa na barafu, lakini kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na joto kuzidi baharini, barafu hiyo imeyayuka na kuwa nyembamba.

Kiasi kwamba meli zinaweza kupita eneo hilo, na na piya viumbe vya baharini vinaweza kuogelea au kuelea na kufika mbali, viumbe kutoka nyangumi hadi mwani.

Mwani huo uitwao Plankton, ni mimea na viumbe vidogo-dogo sana ambavyo ndio chakula kikubwa cha viumbe vya baharini.

Mwani huo wa bahari ya Pacific kuhamia bahari ya Atlantic kunatia wasiwasi juu ya athari yake kwa samaki.

Tayari wanasayansi wameshaona kuwa pwani wa kienyeji katika Atlantic unapotea na pahala pake panachukuliwa na mwani wa kigeni, ambao hautoi lishe nzuri, ikilinganishwa na aina ya asili.

Wanasayansi wanasema hiyo ni sababu moja ya samaki kupungua.