Hali yatengemaa Sudan

Jimbo la Kordofan, Sudan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jimbo la Kordofan, Sudan

Gavana wa jimbo la Sudan la Kordofan Kusini, anasema maisha yanarudi katika hali ya kawaida, baada ya ghasia za majuma kadha.

Gavana huyo, Ahmed Haroun, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, alisema watu waliokimbia wanaanza kurudi.

Mashirika ya kutetea hali za kibinaadamu, yamewalaumu wakuu kuwa kuwa wame-waslazimisha watu kurudi nyumbani, ingawa kulikuwa na mapambano makali baina ya jeshi la serikali, na watu hasa wa kabila la WaNubi.