UN yapigia kura majeshi yake Sudan

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma majeshi ya kutunza amani 4,200 ya Ethiopia katika eneo lenye mzozo la Abyei nchini Sudan.

Jeshi hilo litasimamia kuondoshwa kwa majeshi ya Sudan huko Abyei, na haki za binadamu eneo hilo.

Majeshi ya kaskazini yalidhibiti Abyei mwezi Mei, yaliyozua wasiwasi siku chache kabla ya Sudan Kusini kutangazwa kuwa huru Julai 9.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Abyei

Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia eneo hilo tangu wakati huo.

Azimio hilo limeanzisha jeshi jipya la kutunza amani la umoja wa mataifa, linaloitwa Jeshi la Mpito la Umoja wa Mataifa la Abyei, au UNISFA.

Azimio hilo limepitishwa baada ya mamlaka Khartoum na Juba kutia saini Addis Ababa kuondosha majeshi Abyei na kuyaacha majeshi ya Ethiopia kusimamia amani.

Huku mapigano yakiathiri mataifa jirani ya Kordofan kusini, ghasia Abyei zimezusha wasiwasi baina ya kaskazini na kusini kabla ya pande hizo kutengana.