Nigeria yapata vichochea uchumi

Banki ya ujasiriamali ya Morgan Stanley, imetabiri kuwa uchumi wa Nigeria itakua kwa haraka katika kipindi cha kati, na kuupita ule wa Afrika Kusini ifikapo mwaka 2025 na kuwa yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika. Utabiri huo unakuja wakati uchumi wa Afrika nzima ukianza kuongezeka kwa haraka.

Taarifa ya Morgan Stanley iliyopewa jina 'Uchumi wa Nigeria wapata nguvu ya kuimarika' - inatoa mwangaza kuhusu majaliwa ya nchi hiyo. Taarifa hiyo inatabiri kukuwa kwa asili mia 8 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Goodluck Jonathan

Hali hii, kama inavyosema Benki hiyo, imesababishwa na mambo kadhaa. Muhimu na siyo la kustaajabisha ni bei ya mafuta. Lakini kuna vichochezi vingine pia.

Image caption Umeme waimarishwa

Kati ya hivi ni pamoja na nyongeza ya mishahara kuwaongezea kipato raia wenyewe pamoja na matumaini ya mashirika yanayotoa huduma ya nguvu ya umeme kufanikiwa kuondoa tatizo la umeme.

Benki hiyo inaelezea kuhusu athari za kuyumbayumba kisiasa, lakini kwa sasa hali ni shuari. Taarifa hiyo inatoka wakati gazeti la hapa Uingereza limenukuu Benki ya Uingereza ''Standard chartered bank'' ikitazamia ilichokiita mpasuko wa kukuwa kwa biashara baina ya bara Asia na Afrika katika kipindi cha miaka ishirini ijayo.

Wakati Nigeria na Mataifa mengine ya Kiafrika yakishika kasi ya maendeleo, Afrika kusini itaachwa nyuma,taarifa hiyo inatabiri.