Sita kizimbani Afrika kusini

Raia watatu wa Rwanda Watanzania watatu wamefikishwa kizimbani kwa tuhuma za jaribio la kumuua Lt.Generali Kayumba Nyamwasa.

Image caption Lt.Gen.Kayumba Nyamwasa

Alipigwa risasi katika uti wa mgongo wakati akirejeshwa nyumbani akiwa ndani ya gari mwezi juni mwaka jana lakini alinusurika.

Katika tukio lililosababisha mahusiano baina ya Rwanda na Afrika kusini kudorora, upande wa mashtaka unadai kuwa mmoja wa wanaume aliye kizimbani anamfahamu Bw.Nyamwasa.

Dereva wake, Richard Bachisha, ameondolewa kwenye orodha ya washukiwa kwa sababu licha ya kumfahamu Bw.Nyamwasa, aliwahi kufanya kazi chini ya mkuu huyo nchini Rwanda na baadaye kuwa dereva wake nchini Afrika kusini. Wakati wa tukio yeye ndiye aliyekuwa akiendesha gari.

Vilevile kuna mfanyabiashara aliyetajwa kama kiongozi wa mkumbo huo. Yeye alijaribu kuwahonga polisi wa nchi hiyo dola milioni moja wakati akijaribu kupita uwanja wa ndege wa Oliver TAMBO.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Paul Kagame

Rwanda inamshutumu Bw.Nyamwasa kwa matukio kadhaa ya milipuko mjini Kigali huku Mamlaka za Uhispania na Ufaransa zikidai zinamsaka kuhusiana na uhalifu wa kivita katikati ya miaka ya 90.