United yathibitisha kumsajili De Gea

De Gea Haki miliki ya picha Getty
Image caption De Gea

Manchester United imethibitisha kumsajili kipa David de Gea kutoka Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitano.

Kipa huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Uhispania kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 21, alifanyiwa vipimo vya afya siku ya Jumatatu, kukamilisha uhamisho wake unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 18.9.

"Najivunia sana, na niko tayari kuanza kucheza hapa," amesema De Gea akizungumza na kituo cha televisheni cha Manchester United, MUTV.

"Klabu kubwa kama Manchester United ikikufuata, bila shaka utafurahi sana. Niko makini kufanya niwezavyo kuonesha uwezo wangu." Ameongeza De Gea.

Kukamilika kwa mkataba huo kunamfanya De Gea kuwa kipa wa pili wa gharama zaidi, nyuma ya Gianluigi Buffon ambaye alinunuliwa na Juventus kwa pauni milioni 32.6 mwaka 2001.