DRC yaaga kombe la dunia ya U17 Mexico

Waakilishi wa mwisho wa Afrika katika fainali za kombe la dunia kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamebanduliwa kutoka mashindano hayo, baada ya kufungwa mabao mawili kwa moja na Uruguay.

Haki miliki ya picha Ghetty Images
Image caption DRCU-17 ikichuana na Uruguay katika mechi yao kombe la dunia nchini Mexico

Congo ilitangulia kufunga bao la kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Estadio Morelos ulioko Morelia nchini Mexico.

Uruguay sasa imefuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Mexico na wamepangiwa kuchuana na Uzbekistan ambayo iliifungisha virago Australia.

Licha ya kuondolewa kwenye fainali hizo vijana hao wa Congo walionyesha mchezo mzuri na walishangiliwa sana na mashabiki waliofuriki uwanja huo.

Katika matokeo mengine Brazil imeishinda Ecuador kwa bao moja kwa bila.

Japan ikaiadhibu New Zealand kwa mabao 6-0.