Bashir hataki wapiganaji Kordofan

Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameamrisha jeshi liendelee na shughuli zake katika jimbo la mpakani, la Kordofan Kusini.

Haki miliki ya picha AFP

Rais Bashir alisema jeshi linafaa kuwatimua wapiganaji wa Sudan Kusini katika jimbo hilo.

Sudan Kusini inatarajiwa kupata uhuru juma lijalo.

Matamshi ya Rais Bashir yanaelekea kwenda kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano katika jimbo hilo, yaliyofikiwa mapema juma hili.

Maelfu ya watu wamekimbia Kordofan Kusini tangu mapigano kuzuka mwezi uliopita.