Bashir asema ametimiza ahadi

Rais Bashir aliuambia umati uliohudhuria sherehe za uhuru na viongozi wa kimataifa, kwamba Sudan imetimiza ahadi yake.

Haki miliki ya picha Reuters

Wengi hawakuamini kuwa Khartoum itaiacha Sudan Kusini yenye utajiri wa mafuta, ijitenge.

Na sasa, alisema Rais Bashir, "ni wakati wa Marekani nayo kutimiza ahadi yake, na iondoshe vikwazo dhidi ya Sudan".

Vikwazo hivo vinaleta shida kwa uchumi wa Sudan, ambayo sasa, baada ya Sudan Kusini kupata uhuru, piya imepoteza mafuta mengi.

Rais Bashir piya alitoa wito kuwepo uhusiano wa amani na Sudan Kusini, lakini alikiri kuwa usalama kwenye mpaka wa karibu kilomita elfu mbili baina yao, utakuwa changamoto kubwa.

Lakini alisema mafanikio ya Sudan Kusini yataambatana sana na yale ya Sudan Kaskazini.