Mfumko wa bei umezidi Uchina

Bei ya chakula kupanda nchini Uchina kumezidisha mfumko wa bei kufikia kiwango kikubwa kabisa katika kipindi cha miaka mitatu.

Haki miliki ya picha Reuters

Mfumko ulifikia asili mia 6 nukta 4, katika mwaka uliomalizika mwezi wa Juni.

Upungufu wa nyama ya nguruwe, ulipelekea kiteweo hicho kupanda bei kwa asili mia 50, ikilinganishwa na mwaka jana.

Bidhaa nyengine, zisokuwa chakula, piya zilipanda bei haraka.

Katika mwaka uliopita Uchina ilijaribu kuzimua mfumko wa bei kwa kupandisha kiwango cha riba, na kudhibiti mikopo inayotolewa na mabenki.

Wana-uchumi wengi wanaona kuwa mfumko wa bei sasa ndio umefikia kilele.